Alhamisi 18 Septemba 2025 - 18:10
Ujumbe kutokana na mnasaba wa kupata ubingwa timu ya taifa ya mieleka ya Iran katika mashindano ya dunia

Hawza/ Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iarani, ametuma ujumbe maalumu ukiilenga timu ya taifa ya Mieleka ya Irani baada ya kubeba ubigwa wa duni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Baada ya ubingwa wa timu ya taifa ya mieleka ya ridhaa ya Iran katika mashindano ya dunia ya mwaka 2025, Mtukufu Ayatullah Khamenei katika ujumbe wake alitoa pongezi kutokana na jitihada za kustaajabisha na mwenendo wa mabingwa wa mieleka ya ridhaa wa nchi yetu.

Matini ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:

Bismillahir-Rahmanir-Rahim


Natoa shukurani za dhati kutokana na ubingwa wa dunia wa timu ya mieleka kwa sababu ya jitihada za kustaajabisha na kisha mwenendo mzuri, mchanganyiko wa nguvu na imani umeleta thamani ya juu. Hongereni sana kwenu!

Sayyid Ali Khamenei
25 Shahrivar 1404 Hsh (sawa na Septemba 16, 2025)

Timu ya taifa ya mieleka ya ridhaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya miaka 12, imeshinda ubingwa wa mashindano ya dunia ya mieleka, na ikasajili ubingwa wa sita wa Iran katika historia ya mashindano hayo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha